Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Bulaya adai yeye ni kipenzi cha wana Bunda

 


Mbunge wa Viti Maalum Ester Bulaya, amesema kuwa yeye ni mbunge wa muda mrefu na mbunge kipenzi cha wananchi wa Bunda, ili hali jimbo hilo kwa sasa liko chini ya mbunge Robert Maboto, kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).


Kauli hiyo ameitoa hii leo Februari 9, 2021, Bungeni Dodoma, wakati akiuliza swali kwa Wizara ya Maji kwamba ni lini kata 14 za Bunda zitapa maji safi na salama kupitia mradi wa maji ya kutoka Ziwa Victoria.


"Waziri anajua mradi wa maji wa Bunda umetumia zaidi ya miaka 13, tayari maji yameshatoka Ziwa Victoria na kata 7 za mjini mmeanza kueneza mtandao wa maji. Nataka kujua mimi kama mbunge 'senior' wa eneo lile na kipenzi cha wana Bunda ni lini kata 14 zitapata maji safi na salama", amesema Mbunge Ester


Mara baada ya kauli hiyo, Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson, alionesha kushangazwa na kauli iliyotolewa na mbunge huyo na kuhoji, "Sasa Mheshimiwa Ester, kipenzi cha wana Bunda ni wewe au mbunge wa jimbo la Bunda?".

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments