Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Dereva aliyekimbia ajali iliyosababisha kifo cha Kwitega asakwa na polisi
Dereva wa basi la kampuni ya Makara lililogongana uso kwa uso na gari la aliyekuwa katibu tawala Mkoa wa Arusha, Richard Kwitega anatafutwa na polisi baada ya kutoroka.


Katika ajali hiyo iliyotokea jana, Kwitega alifariki dunia huku watu wanne wakijeruhiwa ambao ni dereva wa Kwitega na wanawake watatu waliokuwa katika basi hilo.Akizungumza na Mwananchi Digital leo Alhamisi Februari 4, 2021 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Harrison Mwakyoma amesema wanamtafuta dereva huyo aliyetoroka baada ya kutokea kwa ajali hiyo."Dereva aliyekuwa anaendesha gari la katibu tawala, Constantine Lubango yupo hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Manyara mjini Babati akiendelea na matibabu ila bado tunamtafuta aliyekuwa anaendesha basi la Makara," amesema Mwakyoma.Amesema bado hawajabaini  chanzo cha ajali hiyo, “tutatoa taarifa kamili ya chanzo cha ajali hiyo mara baada ya uchunguzi wa polisi kukamilika.”Kwa mujibu wa mganga wa hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Manyara, Dk Yesige Mtajwa majeruhi wa ajali hiyo wanaendelea vizuri.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments