Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Fiston Arejea Kuivaa Mtibwa sugar

UONGOZI wa Yanga umewaondoa hofu mashabiki wa timu hiyo kwa kuwaambia kuwa mshambuliaji wao Mrundi, Fiston Abdoul Razack leo atakuwepo kwenye sehemu ya kikosi hicho kitakachowavaa Mtibwa Sugar.

 

Timu hizo zinatarajiwa kuvaana katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa saa moja kamili usiku kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

 

Mrundi huyo hakuwepo sehemu ya kikosi hicho kilichocheza dhidi ya Kagera Sugar mchezo uliomalizika kwa sare ya mabao 3-3 na kuanza kuzua hofu kwa baadhi ya mashabiki wa timu hiyo kuhusu sababu za kutokuwepo kwake.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Ofisa Mhamasishaji wa Klabu ya Yanga, Antonio Nugaz aliweka wazi sababu za kukosekana kwa mkali huyo wa mabao katika mchezo dhidi ya Kagera na kuwahakikishia kuwa nyota huyo atauwasha moto leo.

 

“Hakuna shida yoyote kwa mshambuliaji wa kikosi chetu Fiston Abdoul Razak, na sababu za kukosekana kwake ni kutokana na maamuzi ya mwalimu Kaze kumpumzisha katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar, hii ni kutokana na ratiba yetu ngumu ya kuwa na michezo mitatu ndani ya wiki moja.

 

“Hivyo mashabiki wa Yanga wasiwe na wasiwasi wowote kwani kesho (leo) mwamba Fiston anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi kitakachocheza na Mtibwa Sugar kuendana na maamuzi ya benchi la ufundi, hivyo waje kwa wingi kushuhudia balaa lake,” alisema Nugaz.


 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments