2/07/2021

Godbless Lema Arusha Dongo Bungeni
Godbless Lema, Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema)
LICHA ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa na wabunge kutoka upinzani, Godbless Lemba ambaye alikuwa Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), amesema Watanzania wameanza kukumbuka sauti ya wapinzani bungeni. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Lema anayeishi uhamishoni nchini Canada baada ya kuondoka Tanzania kwa madai ya kuhofia usalama wake, ametoa kauli hiyo tarehe 5 Februari 2021, wakati akizungumzia utendaji wa Bunge la 12 linaloongozwa na Spika Job Ndugai.


Akizungumza kwenye mahojiano na chombo cha Habari cha mtandaoni, Lema amedai Bunge lililoanza hivi karibuni, halina ushawishi kwa wananchi kama mabunge yaliyopita, ambayo yalikuwa na wabunge wengi wa upinzani wa kuchaguliwa.

“Bunge leo umeliona halina hata wiki mbili wala halina mwezi, ndio kwanza limeanza juzi unaona mawazo ya umma kwamba wanaanza kujisikia kuna kitu wame-miss (wamekosa),” amesema Lema.

Katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 28 Oktoba 2020, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilipata viti zaidi ya 360 vya ubunge, huku vyama vya upinzani vikiambulia majimbo 6.

Chadema kilipata jimbo moja saw ana Chama cha Wananchi (CUF), Chama cha ACT-Wazalendo kilipata majimbo menne Zanzibar.

Wabunge wa kuchaguliwa wa CUF ni Shamsia Mtamba, Mtwara Vijijini na Chadema ni Aidah Khenan, Jimbo la Nkasi.

Wabunge wa ACT-Wazalendo ni Khatibu Saidi Haji (Konde), Salum Mohamed Shafi (Chonga), Omar Ali Omar (Wete) na Khalifa Mohamed Issa (Mtambwe).


bunge la tanzania
Kuhusu hatima yake ya kisiasa, Lema amewahakikishia Watanzania kwamba atarejea nchi ni ili kuendeleza mapambano ya demokrasia.

Amesema, demokrasia ya Tanzania haitaimarishwa kwa kufanyika uchaguzi, bali itaimarika kwa kutumia nguvu ya umma, na kwamba hivi karibuni Watanzania wataamua kuhusu hilo.

“Niseme tu kwamba sisi tuko nje ya mipaka, ilibidi tuwe nchini, niwahakikishieni kwamba tutaenda nyumbani wakati ambao muafaka na haiko mbali Watanzania wataamua,” amesema Lema.

Mwanasiasa huyo aliondoka Tanzania kwenda Nairobi nchini Kenya kisha Canada, mwishoni mwa mwaka jana baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu wa 2020.

Lema alidai, kwamba ameamua kuondoka nchini kutokana na kupokea vitisho kutoka kwa watu wasiojulikana.

Hata hivyo, Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Simon Sirro alikanusha kuwepo kwa taarifa za vitisho kwa Lema, alimtaka wanasiasa wengine waliokimbilia nje ya nchi baada ya uchaguzi mkuu, kurudi nyumbani kwani kuna usalama wa kutosha.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

1 comment:

  1. CRBD Wanakutafuta. physical address yako hatujaijua, uko Antwerp.? au umekwenda Sanya Juu?

    ReplyDelete

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger