Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

GSM Yataja Faida za Kocha Mpya Yanga

MKURUGENZI Uwekezaji wa GSM na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Yanga, Injinia Hersi Said, amezitaja faida kuu mbili za kocha wa viungo wa Yanga, Edem Mortotsi.

 

 

Kocha huyo mwenye uraia wa Ghana naCanada, alitambulishwa na Yanga hivi karibuni kuwa kocha wa viungo wa timu hiyo.

 

 

Hersi ameliambia Championi Jumatatu kuwa: “Kocha wetu huyu bado ni kijana mdogo sana, alikuwa mchezaji, lakini malengo yake makubwa ni kuja kuwa kocha wa viungo.

 

 

“Cedric Kaze ambaye ni kocha wetu mkuu, alimpendekeza, sisi tukakaa kumuangalia tukaona anafaa. Tukamleta na yeye akaamua kuachana na kucheza soka ili atimize malengo yake.

 

 

“Kuwa na kocha kama huyu kuna faida kuu mbili, kwanza kama kijana mdogo, atawanoa vizuri wachezaji wetu, lakini kutokana na kuwa kiungo hodari wakati wa kucheza kwake, itakuwa faida nyingine kwa benchi la ufundi atakuwa amekuja kuongeza kitu.”

CAREEN OSCAR,


 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments