Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Ishu ya Ndayiragije Kuchimbishwa Taifa STARS Ngoma Nzito

  


 IKIWA tetesi zinaeleza kuwa Ettiene Ndayiragije, Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzana, Taifa Stars amesitisha mkataba wake, Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF) limesema kuwa lina utaratibu maalumu wa kutoa taarifa.

Ndayiragije alishindwa kukiongoza kikosi cha Stars nchini Cameroon kutinga hatua ya robo fainali kwenye mashindano ya Chan ambayo yanawahusu wachezaji wa ndani nchini Cameroon.


Kutokana na kuboronga huko inaelezwa kuwa amechimbishwa ndani ya Stars ili kuweza kumpata kocha mpya ambaye atakuwa ndani ya Stars.


Stars ilikusanya pointi nne baada ya kucheza mechi tatu, ilishinda moja, sare moja na ilichapwa mechi moja ya ufunguzi kwa mabao 2-0.


Kombe la Chan limekwenda tena nchini Morocco ambao walikuwa ni mabingwa watetezi wa taji hilo ambalo walilitwaa 2018 na kulifanya taifa hilo kutwaa taji hilo mara mbili.


 

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments