Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Kajala Avunja Ukimya Kubeba Mimba ya Harmo
KAJALA Masanja ameendelea kutikisa vyombo vya habari, safari hii amefunguka mambo mengi ikiwemo suala la kumbebea mimba mpenzi wake, Rajabu Abdul ‘Harmonize’, RISASI limezungumza naye.

 

 

Mwanamama huyo ambaye ni ‘pisi’ kali kutoka kiwanda cha Bongo Muvi, amesema kuwa ametukanwa sana kwenye mitandao ya kijamii kuhusu uhusiano wake huo mpya lakini ukweli utabaki palepale kuwa moyo hauendeshwi na hisia za mtu mwingine hivyo wamuache aendelee na mambo yake.

 

 

Mazungumzo yake na RISASI yalikuwa kama ifuatavyo:

Risasi: Kajala naona mambo ya mabodigadi na jeshi siku hizi… Kajala: (Kicheko) nimebidi nicheke.

 

 

Risasi: Vipi lakini unaendeleaje kwenye penzi lako jipya?

Kajala: Niko poa kabisa naendelea kama kawaida na ninafurahi sana penzi langu na sidhani kama kuna anayenidai mimi.

Risasi: Vipi kuhusu maneno ya waja mitandaoni.

 

 

Kajala: Nilishatukanwa sana toka huko nyuma na kwa mambo mengi, hivyo waendelee tu kufanya wawezavyo au kutukana wanavyotaka kwa maana hakuna mtu ambaye anabeba hisia za moyo wangu, waache maisha ya watu wengine yaendelee.

 

 

Risasi: Mna mpango wowote kuhusiana na kufunga ndoa?

Kajala: Kila jambo lina mpangilio na taratibu zake kwa hiyo kama hilo lipo basi litakuja tu.

Risasi: Lakini nakumbuka kama bado ile ndoa ya Katoliki uliyofunga na Chambo kidini bado ipo, maana ndoa za Katoliki hazifunjiki?

Kajala: Ndoa hiyo tulishakamilisha taratibu zote na talaka ilishatoka hivyo sina ninachodaiwa.

 

 

Risasi: Una mpango wa kumbebea mimba na kumzalia Harmonize?

Kajala: Mungu akipenda maana kila kitu ni mpango wa Mungu.

Risasi: Lakini nasikia kama kuna ugomvi wa chinichini wewe na Wolper (Jacqueline)?

 

 

Kajala: Mimi sijajua hilo maana naangalia zaidi mambo yangu, kama kuna mtu ana tatizo na mimi sawa ila mimi niko sawa kabisa.

Risasi: Vipi kuhusu Paula, ishu yake inaendeleaje?

Kajala: Hii ishu iko kwenye mikono ya sheria ndio maana sitaki kuiongelea kabisa kwa sasa.

 

 

Risasi: Unawaambiaje ambao wanakuchamba kuhusiana na malezi ya Paula?

Kajala: Ni ngumu sana kubishana nao kwa sababu mimi ndio ninayejua namleaje mtoto wangu hivyo sitaki kupoteza muda wangu kwenye hilo hata kidogo.

Risasi: Vipi kuhusu shule Paula?

 

 

Kajala: Anaenda hivi karibuni.

Risasi: Haya shukrani.

Kajala: Asante na karibu tena!

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments