Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Kanye West na Kim Kardashian Ndio Basi Tena, Kim Aomba Talaka Rasmi Baada ya Kukosa Maelewano


Rest In Peace KIMYE!! Baada ya panda shuka na nenda rudi za mahakamani, hatimaye Kim Kardshian amefungua rasmi shauri na kudai talaka kwa ajili ya kuachana na Kanye West.

Mtumishi wa Mahakama Kuu ya mjini Los Angeles ameithibitishia CNN kwamba ni kweli Kim Kardashian amewasilisha ombi la talaka na kuiomba Mahakama kumaliza ndoa hiyo iliyodumu kwa miaka 7. Nyaraka zinasema Kim ametoa maelezo kwamba sababu za kuachana ni kukosekana kwa maelewano baina yake na Kanye.


Kwenye shauri hilo pia, Kim ameomba utaratibu wa malezi uwe wa pande zote mbili (Joint Custody) kwa watoto wao Wanne. Imeelezwa kwamba Kanye amesema hana tatizo na mfumo huo wa malezi na yupo tayari kushirikiana na Kim kuwalea pamoja (Co-parenting) watoto wao.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments