Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Kasi ya Simba Yampa Presha Cedric Kaze Yanga

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mrundi, Cedric Kaze amefi chua kuwa kwa sasa wamekuwa kwenye presha kubwa ya kuhakikisha wanapata matokeo katika kila mchezo kutokana na kasi ya wapinzani wao wakiwemo Simba kuelekea kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

 

Kaze ametoa kauli hiyo ikiwa Yanga inaongoza ligi kwa pointi 49, ikifuatiwa na Simba wenye pointi 42 huku wakifuatiwa na Azam wakiwa na pointi 36.

Akizungumza na Championi Jumatano,Kaze alisema kuwa matokeo wanayopata kwa sasa yamekuwa yakiongeza presha kwao lakini wataendelea kupambana kwa kuhakikisha wanafi kia malengo.“Hatujawa kwenye kipindi kizuri kwa sasa hasa upande wa matokeo, presha imekuwa kubwa upande wetu kwa sababu kila aliyekuwa nje anataka kuona matokeo mazuri na hilo ndiyo lengo letu kuona tunafanya hivyo.

 

“Kikubwa tunachokiangalia ni malengo ya timu kuweza kufi kiwa kwa pamoja na kuweza kuondoa presha ambayo tumekuwa nayo kwa sasa kutokana na matokeo ya mechi ambazo zimepita na kasi kubwa ambayo wamekuwa nayo wapinzani (Simba), wetu ambao wamekuwa wakishinda michezo yao mfululizo,” alisema Kaze.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments