Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Kenya yawazuia wanariadha wake kushiriki Kimanjaro Marathon

Kenya imekataa kuwaidhinisha wanariadha wake kushiriki mbio za masafa marefu za Kilimanjaro Marathon nchini Tanzania kwa kuhofia janga la corona.
Mashindano hayo yanayotambuliwa na Shirikisho la Riadha Duniani IAAF- yataandaliwa e Jumapili hii chini ya mlima Kilimanjaro, mlima mrefu zaidi barani Afrika.

Wanariadha wa Kenya wamekuwa wakitawala mbio hizo katika makala yaliopita.

Katika taarifa, Shirikisho la Riadha la Kenya limetoa wito kwa "wanariadha wote kutosafiri Tanzania kushiriki mashindano hayo".

Tanzania haijakuwa ikitoa data ya hali ya corona nchini humo tangu kati kati ya mwaka jana.

Mapema wiki hii Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitoa wito kwa Tanzania kuanza kutoa data ya watu walioambukizwa virusi vya corona.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments