Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Kigogo Yanga Afungukia Mkataba wa Carlinhos Kumalizika


BAADA ya kiungo wa Yanga, Carlos Carlinhos kuwa nje kwa muda mrefu huku zikienea tetesi kuwa huenda mchezaji huyo akaachwa mwishoni wa msimu huu, hatimaye bosi wa Yanga, Injinia Hersi Said amefunguka kuwa kiungo huyo bado yupo ndani ya timu hiyo.

Carlinhos mwenye uraia wa Angola alijiunga na Yanga katika usajili wa dirisha kubwa mwanzoni mwa msimu huu ambapo amekuwa akipatwa na majeraha ya mara kwa mara kiasi cha kukosa mechi nyingi.

Hersi ambaye pia ni Mwenyekiti Msaidizi wa Kamati ya Usajili wa Yanga na Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Kampuni ya GSM, amesema mchezaji huyo wakati anasajiliwa na Yanga alisaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu, hivyo wanatarajia kumuona akiendelea kucheza ndani ya timu hiyo mpaka mwisho wa mkataba wake na wala hawana mpango wa kumuacha.

“Carlinhos wakati anatua Yanga alisaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu wa kuitumikia Yanga, hivyo ndiyo kwanza ameutumikia nusu mwaka, kabakiza mwaka mzima wa kuendelea kucheza na tunatarajia kumuona akiendelea kuichezea Yanga na si kumuacha kama navyosikia.“

Kibaya kwake ni majeraha ambayo amekuwa akiyapata lakini ni moja kati ya wachezaji wazuri ambao tumejaliwa kuwa nao ndani ya timu yetu, sisi kama viongozi tunaamini kupitia mzunguko wa pili atafanya mambo makubwa na ndiyo maana bado tunamuamini kuwa atatusaidia,” alisema kiongozi huyo.

NA MARCO MZUMBE, Dar es Salaam -Championi

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments