2/13/2021

Kocha Simba: Ushindi tulioupata ni mwanzo mzuri katika kutimiza adhima yetu ya kufanya vizuri
KOCHA mkuu wa klabu ya Simba, Didier Gomes Da Rosa amefunguka kuwa ushindi walioupata dhidi ya AS Vita kwenye mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ni mwanzo mzuri kwao kufanya vizuri zaidi katika michuano hiyo mwaka huu.
Simba jana usiku iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji wao AS Vita, katika mchezo wa kwanza wa kundi A uliofanyika katika Stade Des Martyrs, Kinshasa nchini Congo.

Ushindi huo umeifanya Simba kuongoza msimamo wa kundi A wakiwa na pointi zao tatu na faida ya bao moja, ambapo wanasubiri kuona matokeo ya mchezo wa Al Ahly na Al Merrikh.

Akizungumzia furaha yao baada ya ushindi huo dhidi ya AS Vita Gomes amesema: “Tumefurahi sana na tumeridhishwa sababu tulicheza vizuri na matokeo ni mazuri.

"Kwa Simba matokeo haya yatakuwa na faida mbeleni katika hatua hii ya makundi na katika kutimiza adhima yetu ya kufanya vizuri,"

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger