Korea Kaskazini yashtumiwa kwa wizi wa data za utengenezaji wa chanjo ya corona

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


Korea Kaskazini imenaswa ikijaribu kuiba teknolojia inayotumika kutengeneza chanjo ya virusi vya corona kutoka kampuni ya utengenezaji dawa ya Marekani, Pfizer, kulingana na maafisa wa kijasusi wa Korea Kusini.

Hadi kufikia sasa haijabainika ni taarifa gani hasa ambazo zimeibwa.


Shirika la kijasusi la taifa la Korea Kusini limechukua hatua binafsi na kutaarifu wabunge juu ya kinachodaiwa kuwa uvamizi, kulingana na shirika la habari la eneo la Yonhap.


Hadi sasa kampuni ya Pfizer kufikia sasa bado haijasema lolote.


Korea Kaskazini bado haijawahi kuripoti hata kisa kimoja cha maambukizi ya ugonjwa wa virusi vya corona.


Hata hivyo, nchi hiyo inatarajiwa kupokea dozi milioni 2 za chanjo ya AstraZeneca wiki chache zijazo.


Korea Kaskazini ilifunga mipaka yake Januari, mwaka jana muda mfupi baada ya ugonjwa wa virusi vya corona kuanza kujitokeza nchini China.


Novemba, Mwaka Jana kampuni ya Microsoft ilisema takribani mashirika 9 ikiwemo Pfizer zilikuwa yamelengwa na mashirika yanayoungwa mkono na serikali nchini Korea Kaskazini na Urusi.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad