6/11/2022

Kutana na Mwanamke Sara Baartman Mwanamke Aliyetumika Kivutio Cha Maonesho Uingereza Sababu ya Makalio Makubwa

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


Pichani ni Sara Baartman mzaliwa wa Afrika Kusini kutoka katika kabila la Khoikhoi. Alizaliwa mnamo mwaka 1789.

Sara alikuwa ni mwanamke mwenye maumbile makubwa na yenye kuvutia, hususani makalio yake kama jinsi inavyoonekana pichani.

Umbo lake liliwavutia sana Wazungu. Kutokana na umbo lake hilo mwaka 1810 Wazungu walimchukua na kumpeleka Uingereza ambapo alitumika kwa kufanyiwa maonyesho jukwaani na kuwaingizia pesa Wazungu hao.

Mwaka 1814 alihamishiwa Ufaransa ambako pia alikuwa akifanyiwa maonyesho akiwa uchi. Watu walikuwa wakimuita Hottentot Venus (mungu wa mapenzi wa khoikhoi). Sarah alifariki mwaka 1815 akiwa na miaka 26 na inasemekana alikufa kwa ugonjwa wa zinaa unaoitwa Kaswende (syphilis).

Mabaki ya mwili wake kama fuvu pamoja na sehemu zake nyeti ziliendelea kufanyiwa maonyesho katika makumbusho huko Paris, Ufaransa hadi miaka ya 1970's. Mwaka 2002 mabaki hayo yalizikwa.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger