Kiongozi wa Al-Qaeda nchini Yemen adaiwa kukamatwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


Umoja wa Mataifa (UN) ulitangaza kuwa kiongozi wa shirika la kigaidi la Al-Qaeda nchini Yemen, Khalid Batarfi, alikamatwa akiwa hai miezi kadhaa iliyopita.
Ndani ya wigo wa UN, "wataalam wanaohusika na ufuatiliaji wa makundi yenye msimamo mkali" walichapisha ripoti juu ya suala hilo.

Katika ripoti hiyo, iliarifiwa kwamba Batarfi, anayejulikana kama "Abu Mikdad al-Kindi", alikamatwa akiwa hai kwenye operesheni iliyoendeshwa  El-Gayda, katikati mwa mkoa wa Al-Mehra, mnamo Oktoba mwaka jana, ambapo naibu wake Saad bin Atıf al-Awlaki aliuawa wakati wa operesheni hiyo.

Wakati hakuna taarifa yoyote iliyotolewa katika ripoti hiyo kuhusu maelezo ya wahusika wa walioendesha operesheni hiyo, vyanzo vya Yemen vinasisitiza kuna uwezekano operesheni hiyo iliendeshwa na vikosi vya Saudi Arabia vilivyohudumu Mehra kwa miaka mingi.

Khalid Batarfi alichukuwa nafasi kama kiongozi wa shirika hilo baada ya Qassem er-Rimi, ambaye alikuwa kiongozi wa Al-Qaeda katika Rasi ya Arabia kuuawa mnamo Januari 2020 kwenye  shambulizi la chombo cha anga kinachojiendesha cha Marekani.

Batarfi alitoroka na watu wapatao 300 baada ya uvamizi wa gereza katika mkoa wa Hadramawt nchini Yemen mnamo Aprili 2015.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad