Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Makabubri yanayoashiria unyama uliofanywa na 'Familia ya Jehanamu' Libya
Hadi msimu wa joto uliyopita, ndugu hao wa Kani waliudhibiti mji mdogo Libya, kuwaua wanaume , wanawake na watoto kudumisha mamlaka yao.


Sasa uhalifu wao umeanza kufichuliwa pole pole.Kwa miaka saba wafanyakazi, waliovalia suti nyeupe za kujilinda dhidi ya kemikali wamekuwa wakirejea katika mji mdogo wa kilimo Tarhuna, uliopo kusini- mashariki mwa mji kuu wa Libya, Tripoli.Wameweka alama katika ploti ambazo wametoa miili 120 kwa kutumia tepu nyekundu na nyeupe japo sehemu kubwa ya ardhi hiyo haijaguswa."Kila wakati ninapochimba mwili mpya, najaribu kufanya hivyo kwa umakini kadri ya uwezo wangu," anasema mmoja wa wafanyakazi wa, Wadah al-Keesh. "Tunaamini kwamba tukivunja mfupa, roho yake itasikia."Baadhi ya miili hiyo inasadikiwa kuwa ya wapiganaji wadogo waliouawa vitani karibu na Tarhuna msimu uliyopita wa joto, katika mwaka wa tisa wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Libya.Lakini wengi wao ni raia - wakiwemo wanawake na watoto wadogo waliyo na umri wa hadi maka mitano - baadhi yao wakiwa na alama za kuteswa.Makaburi hayo ni ishara inayoangazia utawala wa ugaidi uliyodumu kwa karibu miaka minane, ukiendeshwa na familia ya Kanis, na wanamgambo wao.Watatu kati ya ndugu saba wa Kani wamefariki, na wengine walitoroka mwezi Juni mwaka 2020 bade ya kushambuliwa na vikosi tiifu kwa Serikali ya Muungano ya Libya(GNU) inayotambuliwa na Umoja wa mataifa, lakini mpaka sasa wakazi wa Tarhuna wanaogopa kuzungumzia uhalifu wao.Baadhi yao wanasema kuwa wanatishiwa na wafuasi wa ndugu wa Kani.Kukusanya pamoja taarifa kuwahusu ndugu hao - Abdul-Khaliq, Mohammed, Muammar, Abdul-Rahim, Mohsen, Ali na Abdul-Adhim sio mambo rahisi.Lakini kutokana na simulizi za kuogofya kutoka kwa watu waliowajua, familia hiyo masikini ilitumia ghasia iliyokumba Libya baada ya mapinduzi ya mwaka 2011 dhidi ya, Kanali Muammar Gaddafi - na kuongoza jamii yao kwa kutumia ukatili mkubwa."Ndugu hao saba walikuwa wabaya sana na wala hawakuwa na ustaarabu katika jamii," anasema Hamza Dila'ab, wakili na mwanaharakati wa kijamii, ambaye anakumbuka kukutana nao katika maharusi na mazishi kabla ya mwaka 2011.Mapinduzi yalipofanyika, watu wengi katika mji wa Tarhuna walisalia kuwa watiifu kwa Gaddafi.Koingozi huyo wa kiimla aliupendelea sana mji huo, kwa kuwapatia wanaume kutoka familia kubwa kazi nzuri katika vikosi vyake vya usalama.Familia ya Kani ilikuwa miongoni mwa watu wachache waliounga mkono mapinduzi - lakini sio kwa maslahi ya wananchi, anasema Hamza Dila'ab, bali ni kutokana na uhasama wa miaka 30 kati yao na ndugu wa familia ya wafuasi wa Gaddafi.Baada ya kung'olewa madarakani kwa Gaddafi, ndugu hao walipata nafasi ya kutekeleza maovu yao." Ndugu wa Kani walifanikiwa kuua familia hiyo kisiri mmoja baada ya mwingine ," anasema Hamza Dila'ab.Lakini msururu huo wa mauaji ya kulipiza kisasi ilichangia kuawa kwa ndugu mdogo wa Kani, aliyefahamika kama Ali mwaka 2012."Ali alikuwa ndugu mdogo mtanashati wa Kani, na alipofariki,alimfanya shujaa,"anasema Jalel Harchaoui, mtaalamu wa Libya katika taasisi ya Clingendael nchini Uholanzi, ambaye alifanya utafiti wa historia ya familia hiyo."Ndugu hao waliamua kulipiza kisasi kifo chake sio tu kwa kuwasaka waliohusika na mauaji yake na kuwaua. Walichofanya ni kuangamiza familia yao yote ."Familia ya Kani iliendelea mbele kwa kuimarisha vikosi vilivyokuwepo mjini humo na kabuni vikosi vyao vipya vya wanamgambo vilivyojumuisha maelfu ya wapiganaji.Sawa na wanamgambo wengine nchini Libya walipata ufadhili kutoka kwa serkali. Na kuachana na suala la kulipiza kisasi huku ndugu walisalia wakitumia mamlaka yao kikamilifu mjini Tarhuna."Sera ilikuwa ni kuwatesa watu kwa lengo la kuwaogopesha. Waliwaua watu kinyama ili kutimiza lengo hilo. Mtu yeyote mjini Tarhuna ambaye aliwapinga alikumbana na mauti," anasema Hamza Dila'ab.Hanan Abu-Kleish alikuwa nyumbani Aprili 17 mwaka 2017 wakati wanamgambo wa Kani walipowavamia."Mmoja wao aliniwekea bunduki kichwani," anasema. "aliniuliza ni nani yuko nyumbani, nikamwambia, ' akuna mtu.' Lakini aliniburuza chini na na kunipeleka chumbani kwa baba yangu. wakamwambia: ' utakuua wewe kwanza.' Na bila lusitanien wakamuua. Nilijaribu kuwazua lakini walimmiminia risasi kifuani."Ndugu watatu wa kiume wa Hanan pia waliawa siku hiyo pamoja na watoto wao wawili waliyokuwa na umri wa miaka 14 na 16.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments