Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Mambosasa: Tumemkamata “Anayejiita Askofu” Mwamakula

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es Salaam limemkamata Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula wa Kanisa la Uamsho la Moravian kwa kosa la kuhamasisha maandamano Nchi nzima kupitia mitandao ya kijamii.

 

Kamanda Mambosasa amesema taarifa ya Mwamakula ilikuwa ikihamasisha Wananchi wajitokeze kwa wingi ili kuandamana wakishinikiza na kudai #Katiba mpya jambo ambalo ni kinyume na taratibu na Sheria za nchi.

 

Amesema Polisi kupitia Idara ya Upelelezi Kanda Maalum Dar es Salaam walifanikiwa kupata taarifa hiyo na kumkamata Askofu Mwamakula kwaajili mahojiano kwa jambo hilo lililoelezwa kuleta taharuki kwa Umma.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments