Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Mameneja wawili TANESCO wasimamishwa kwa kutokuwepo maeneo ya kazi


Waziri wa Nishati, Medard Kalemani amewasimisha kazi vigogo wawili wanaosimamia vituo vya kuzalisha umeme vya Ubungo 1 na Kinyerezi 1.


Waliosimamishwa kazi ni Meneja wa Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Ubungo 1, Nkulungwa Chanumba na Meneja wa Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Kinyerezi 1, Marco Zakaria kutokana na kile alichokiita kuhujumu uzalishwaji wa umeme kwenye vituo vyao.


Meneja wa kuzalisha umeme wa Ubungo 1 amesimamishwa kazi kwa kutokuwepo kwenye eneo lake la kazi bila kutoa taarifa kwa wakubwa zake wakati Meneja wa Kinyerezi 1 yeye hakuwepo kwenye eneo la kazi wakati utengenezwaji wa dharura wa mtambo wake ukifanyika.


Kutokana na kadhia hiyo Kalemani amemuagiza Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati kuunda kamati ya uchunguzi dhidi ya watumishi hao wawili na kuitaka impatie taarifa ndani ya siku 14 na kuwa ikibainika kufanya hujuma wafikishwe mahakamani.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments