Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Marekani ipo ''kwenye mazungumzo'' kuhusu kesi ya Rusesabagina

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

 


Kesi ya Paul Rusesabagina, mfanyakazi wa hoteli aliyeitwa shujaa kwenye filamu ya Hollywood kuhusu mauaji ya kimbari nchini Rwanda, Hotel Rwanda, inaanza leo.

Anashtakiwa kwa makosa ya ugaidi, mauaji na uhalifu mwingine. Mawakili wake wamekana mashtaka hayo dhidi yake.


Wizara ya mambo ya nje ya Marekani ilisema siku ya Alhamisi kuwa


imeshirikiana na serikali ya Rwanda katika "kwa kiasi kikubwa" huko "Washington na pia Kigali".


‘’Tunaamini mchakato wa kisheria utakuwa wa haki na uwazi, utakaoheshimu utawala wa sheria, na unaokwenda sawa na kuwajibika kwa Rwanda katika kuheshima haki za kimataifa za binadamu. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje Ned Price aliwaambia waandishi wa habari.


Bwana Rusesabagina ni mkosoaji mkubwa wa Rais Paul Kagame, na amekuwa akiishi uhamishoni nchini Marekani.

Post a Comment

0 Comments