Mbunge Afunguka "Kama Serikali Inataka Kutengeneza Watu Mabilionea Basi iache Kufunga Account za Watu Wanaokutwa na Hela Nyingi"


Mh. Rais kwenye hotuba amesema tutengeneze Mabilionea na tusiogope, jambo la kwanza ambalo tunatakiwa tusiogope ni tusiogope kusema uhalisia.. nasikitika sana kule Mafinga unakuta Mtu kauza miti yake MILIONI 300 au 400 kuna kuja sijui Task Force I don’t know whatever you call it alafu account inafungwa”


“Mimi nilitarajia kwamba wangekua wanauliza wewe Kosato kwanini unafanya biashara wakati account haina hata milioni 5? lakini usiniulize don’t ask me kwanini nina milioni 500, wewe tafuta mbinu zako za kiserikali angalia je hii milioni 500 ya Chumi ni safi au sio safi lakini ukinifungia mimi Akaunti tutatengenezaje Mabilionea?”


“Leo hii pale Mafinga tozo kwenye sekta ya mazao ya misitu zipo 13 Viwanda vitano vimefungwa, imagine kama Kiwanda kimoja kinaajiri Watu 300 tayari Watu 1500 hawana ajira na pia Serikali inakosa kodi za SDL, PAYE, kwahiyo katika kumsaidia Mh. Rais na Serikali ni lazima tuwe wakweli wa nafsi” —— Mbunge wa Mafinga Mjini Cosato Chumi. #MillardAyoBUNGENI

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE