Mbunge ‘Ajichanganya’, JPM Aagiza Uchunguzi wa Bil 19

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA





Rais wa Tanzania, John Magufuli ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuchunguza mkopo wa Sh19 bilioni uliotolewa na benki ya CRDB kwa halmashauri ya Temeke.

 

 

Kiongozi mkuu huyo wa nchi ametoa agizo hilo leo Ijumaa Februari 26, 2021 katika ziara yake jijini Dar es Salaam baada ya mbunge wa Temeke (CCM), Dorothy Kilave kuomba Serikali iwasaidie kulipa mkopo huo unaowagharimu Sh4.8 bilioni kila mwaka.

 

 

“Yaani Serikali ikalipe mkopo ambao haikuhusika, haya ni mambo ya ajabu. Mlienda kuzungumza wenyewe na benki mmeshindwa kulipa mnataka Serikali ilipe. Kuna manispaa ngapi kwa hiyo ziwe zinafanya mikopo ya wizi halafu serikali ilipe. Hilo mtalibeba wenyewe, kwanza ni kukosa nidhamu.”

 

 

“Hakuna hela itakayotolewa na serikali labda kutuma wachunguzi kuchunguza kujua hizo fedha zinarushwa kiasi gani, namuelekeza kamanda wa Takukuru kuchunguza hawa naona kuna ufisadi mkubwa unaelea,” amesema Magufuli.

 

 

Amesema hiyo ilikuwa kawaida ya halmashauri kujiingiza kwenye ufisadi na kutumia vibaya fedha za miradi.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad