Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Mbunge amwagiza Polepole awapelekee CCM ujumbe huu

 


Mbunge wa Konde kupitia Chama cha ACT Wazalendo Khatib Haji, amemwagiza Mbunge wa kuteuliwa Humphrey Polepole, aende akawaambie wana CCM ambao bado wanataka Rais Dkt. Magufuli, aongeze muda wa madarakani kwamba alikwishasema hawezi kuongeza muda hivyo wasimlazimishe.


Kauli hiyo ameitoa hii leo Februari 9, 2021, Bungeni Dodoma, wakati akitoa pongezi kwa Rais Dkt. Magufuli, kwa kuamua kuiheshimu na kuilinda katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo licha ya wanachama wenzake kutaka asiondoke madarakani lakini yeye amekwishaweka msimamo wake siku nyingi kwamba akimaliza wamu zake ataondoka.


"Magufuli atakuwa ni Rais wa kwanza kwa nchi za Afrika ambaye baadhi ya wabunge wake wanamuomba aongeze muda lakini tayari ameweka msimamo. Polepole waambie CCM Rais hana shida ya kuongeza muda alikutuma na video zinatembea tunaziona kwanini unawaacha akina Sanga hapa wanaendelea kupotosha?, kwanini hamuheshimu mawazo ya Mh. Rais?", amesema Mbunge Khatibu.


Akijibu hoja hiyo Polepole amesema kuwa, "Mimi naomba nitumie nafasi hii kumpa taarifa Mbunge, kwamba masuala ya CCM yanzungumziwa kwenye vikao vya chama hapa Bungeni, wabunge wana uhuru wa kutumia uhuru wa Bunge kuzungumza lakini kinachozungumzwa hapa ndani hakiathiri msimamo wa chama tumekwishautoa Rais hataongeza muda".

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments