Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Mchekeshaji maarufu nchini Marekani Kevin Hart Amburuza Mfanyakazi Wake Mahakani Kwa Kumuibia Bilioni 2.7


Mwaka 2015 Mchekeshaji maarufu nchini Marekani Kevin Hart alimuajiri Dylan Syer kama mfanyakazi wake ambaye atakuwa akimfanyia shughuli zote za manunuzi ya vitu mbali mbali. Hart alimruhusu hadi kutumia Kadi yake ya Kibenki (Credit Card) kwa ajili ya kufanya manunuzi hayo.


Sasa taarifa iliyotoka leo ni kwamba mchekeshaji huyo amemfikisha mahakamani Syer akidai kuwa amemuibia kiasi cha ($1.2M) takribani TSh. Bilioni 2.7 toka kwenye akaunti yake ya benki ambapo inaelezwa Syer alikuwa akichota tu fedha na kuzihamishia kwenye akaunti yake binafsi na kuandika ripoti kuwa ametoa fedha kwa ajili ya manunuzi.


Inaarifiwa kwamba kijana huyo alitumia kiasi cha ($400K) takribani TSh. Milioni 900 kwa kununua Saa kadhaa za mkononi, pia aliitumia pesa ya Kevin Hart ipasavyo kwa kununua mabegi ya Louis Vuitton, midoli ya kuchezea na vitu kedekede vyenye thamani.


 DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE

Maofisa wanaeleza kwamba, Hart alipigwa na kijana huyo kiasi cha ($1 million) takribani TSh. Bilioni 2.3 katika kipindi cha miaka miwili pekee.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments