Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Mchekeshaji TrevorNoah Anunua Jumba Lenye Gharama ya Bilioni 64

 


Wakati Wachaga wakiwa Moshi Disemba 2020 wakitamba kwa kuangusha mbuzi na vikombe vya mbege, Mchekeshaji #TrevorNoah alikuwa mjini Los Angeles akifanya manunuzi ya Jumba la Kifahari.


Mchekeshaji huyo raia wa Afrika Kusini alinunua Jumba la Kifahari kwenye makazi ya Bel Air mjini Los Angeles California, kwa kiasi cha ($27.5 million) sawa na Bilioni 64.9 za Kitanzania, SWIPE kuitazama vizuri.


Hili sio jumba la kwanza kununua mitaa hiyo, 2018 alifanya hivyo kwa kutoa kitita cha ($20.5 million) lakini aliishia kuliuza jumba hilo September 2020 kwa ($21.7 million). Noah (36) ni mchekeshaji, Mwigizaji na mtangazaji wa televisheni, akitamba na kipindi chake maarufu kiitwacho The Daily Show.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments