Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Mchezaji Bwalya Afunguka "Nitalipiza Kisasi Cha Kufungwa na Simba Wakati Nacheza Nkana"MSHAMBULIAJI wa klabu ya Al Ahly, Walter Bwalya amefunguka kuwa amejipanga kuhakikisha analipa kisasi cha kufungwa na Simba wakati akiwa nahodha wa Nkana, pale Al Ahly itakapokutana na Simba katika mchezo wa hatua ya makundi ya Ligi ya mabingwa Afrika.


Bwalya amewahi kuja nchini na kikosi cha klabu ya Nkana ya Zambia, na kucheza dhidi ya Simba katika mchezo wa raundi ya kwanza uliopigwa Desemba 23, mwaka 2018 ambapo alifanikiwa kumtungua kipa wa Simba Aishi Manula dakika ya 17 ya mchezo.


Licha ya bao hilo la kuongoza mchezo huo uliisha kwa Nkana kupoteza kwa mabao 3-1 na Simba kutinga hatua ya makundi.


Nyota huyo juzi alishindwa kufurukuta katika mchezo wa nusu fainali ya klabu bingwa dunia na kushuhudia kikosi chake kikipokea kipigo cha mabao 2-0.


Bwalya alijiunga rasmi na Al Ahly katika kipindi cha dirisha dogo na kutambulishwa Desemba 31 mwaka jana, ambapo alisaini kandarasi ya miaka minne kuwatumikia Mafarao hao.


Akizungumzia mchezo dhidi ya Simba, Bwalya amesema: "Nafurahi kupata fursa ya kukutana tena na Simba ili niweze kulipa kisasi juu ya kumbukumbu mbaya wakati nikiwa Nkana, naamini nitatumia mchezo huo kulipa kisasi," 

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments