Mkataba wa Messi wavuja, Barca wageuka mbogo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Barcelona imesema kuwa itachukua “hatua za kisheria” dhidi ya gazeti la Uhispania la El Mundo baada ya kuchapisha maelezo kuhusu mkataba wa mshambuliaji, Lionel Messi wa pauni milioni 492.

Barcelona vs Bayern Munich: End Of An Era As Barca Humiliation Makes  Revolution The Only Option | Football News

Barcelona ilikanusha kuhusika kwa namna yoyote ile katika uchapishaji wa taarifa hizo. Kwa mujibu wa El Mundo, mkataba wa Messi wa miaka minne ulikuwa wa thamani ya takriban euro 555,237,619 hadi Juni 30, 2021.

Hii inamaanisha kuwa kijana huyo mwenye umri wa miaka 33, atakuwa anapokea pauni milioni 123 kwa msimu.

Barcelona imesema katika taarifa iliyotoa kuwa “inasikitishwa na uchapishaji wa maelezo hayo”. Na kuongeza kuwa: “FC Barcelona haihusiki kwa namna yoyote ile katika uchapishaji wa taarifa hiyo na itachukua hatua stahiki za kisheria dhidi ya gazeti la El Mundo, kwa uharibifu wowote ule ambao huenda umetokea kwasababu ya taarifa hiyo.

“FC Barcelona imeonesha kumuunga mkono Lionel Messi, hasa katika jaribio lolote la kumdhalilisha na kuharibu uhusiano wake katika klabu hiyo ambako amefanyakazi na kuwa mchezaji bora duniani na katika historia ya soka.”

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina Messi alijiunga na Barcelona akiwa na umri wa miaka 13 lakini akatuma ombi la kutaka aruhusiwe kuhamia kwingineko mnamo mwezi Agosti.

Bado haijafahamiki ikiwa atabaki katika klabu hiyo wakati mkataba wake utakapomalizika.

Messi ni mchezaji wa Barcelona aliyeweka rekodi katika ufungaji wa magoli mengi na ameshinda makombe 10 ya La Liga, Ligi ya mabingwa mara nne na tuzo ya Ballon d’Or – alipewa tuzo mara sita ya mchezaji bora duniani.

Ombi lake la kutaka kuondoka Barcelona lilifuatiwa na kutoelewana kati yake na rais wa klabu hiyo Josep Maria Bartomeu, aliyeacha kazi hiyo mnamo mwezi Oktoba.

Messi, anayeelezea utawala wa Bartomeu kama “janga”, alisema mnamo mwezi Desemba “Bado sijajua nitakachofanya.”

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad