Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Mke wa Method Man Amjibu Wendy Williams Baada ya Kudai Alifanya Mapenzi na Mume Wake

 


Mke wa rapa Method Man ameamua kuvunja ukimya juu ya madai ya mtangazaji Wendy Williams ambaye hivi karibuni kupitia mahojiano na DJ Suss, aliibuka na kusema aliwahi kufanya mapenzi na Method Man mara baada ya kukutana kwa usiku mmoja miaka ya 90.


"Tulivuta bangi sana pamoja kwenye Jacuzzi na [Method Man] wakati nikimuogesha na ilikuwa ni kitendo cha usiku mmoja tu yaani (One Night Stand)" alisema Mwanamama huyo na kukiri kuwa walienda mbali zaidi hadi kukutana kimwili.


Lakini madai haya kama hayaingii vizuri kwenye akili ya mke wa Method Man, Tamika Smith ambaye ameibuka kwenye ukurasa wake wa Instagram na kumshambulia vikali mtangazaji huyo maarufu akimuita mgonjwa, na miongoni mwa makahaba wakubwa kuwahi kutokea kwenye sayari hii.


"Kwa miaka sasa, nimekuwa kimya pale ambapo Wendy Williams amekuwa akianzisha mashambulizi dhidi ya mume wangu, mimi binafsi na familia yetu. Kipindi cha nyuma nilikuwa napuuzia uongo wake dhidi yetu. Uchu wake na maisha yetu umefika pabaya sana. Na nimechoka kuwa mkimya." alianza kwa kusema Tamika ambaye amedumu kwenye ndoa na Method Man kwa miaka 20 sasa.


"Ukiachilia mbali hasira zangu, nilichagua kutomjibu hadharani kutokana na madai yake yasiyo na afya dhidi ya mume wangu na ndoa yetu. Ni dhahiri kwamba alikuwa mgonjwa na alikuwa akipambana na tatizo la chuki na kutojitambua." alikazia Tamika na kumalizia kwamba Wendy anasumbuliwa na dawa za kulevya na ndio maana amekuwa na muonekano mbaya nje na hata ndani ya mwili wake. Hivyo chuki na kusema watu ndio nafuu kwake kwa sasa.


Akizungumzia ndoa yake Tamika alisema "Kuweka sawa tu, ndoa yangu ni imara, mume wangu anaendelea kufurahia matunda ya kazi yake, na Wendy milele ataendelea kuwa miongoni mwa makahaba wenye maisha mabovu kwenye hii sayari."


 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments