Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Mobeto: Kajala Acha Uongo, Hili Litakuwa Fundisho Kwa Wanaopenda Kunisingizia Vitu

 


MSANII wa Bongo Fleva na mwanamitindo, Hamisa Mobetto amesema amechoshwa na baadhi ya watu kumlaumu na kumsingizia mambo ambayo amedai binafsi hayajui wala hayamuhusu.


Kauli hiyo ya Mobetto imekuja muda mfupi baada ya msanii mwenzake, Kajala Masanja kumtuhumu kuwa alimchukua Kajala na kumpeleka kwa Rayvanny ili wakajiachie kimahaba na kisha kurekodi video ya kuisambaza mitandaoni.


Jamani hata kama HAMISA MOBETTO ndio jumba bovu lenu la kutupia takataka ifike mahala ifike ukomo. Siamini kama baada ya kukaa na kutafakari cha kuexplain kuhusu haya mmeona mimi ndio ninaweza kuwa Damage Controller.


Kajala hiyo tarehe 9 mwanao aliniomba nimtoe Lunch, nikamwambia inabidi niongee na wewe kwanza, na nikakupigia ukaona ni sawa tu.Nilimtoa Lunch na muda wote nilikua naongea na wewe kwenye simu mpaka nimemrudisha hapo Gym kwako Mimi mwenyewe soon after lunch. Na huoni Kama unaongea uongo hadharani bila woga??


Siku ninatoka na Paula alikuwa na nywele hizo za kwenye videos? Naomba nilaumiwe kwa kukubali ombi la kumpeleka mwanao lunch na si vinginevyo.Mimi ni Mama, mfanya biashara, mdau na balozi wa makampuni mbali mbali. Brand yangu nimeijenga kwa muda mrefu hivyo ningependa iheshimike na isichafuliwe kwa shutuma za uongo kama hizi.


Mimi pia ni mzazi na mtoto kwa mama yangu kama ilivyo wewe. Nimeona nisafishe upepo mchafu huu uliouelekezea kwangu siku hii ya wapendanao, lakini zaidi you’ll hear from my lawyer.


 DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE

Rest assured sitaliacha hili lipite bure, nafikiri itakuwa fundisho zuri na kwa wale wooooote ambao wamekua wakichafua jina langu kwa upuuzi wao.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments