Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Morrison, Mugalu Gumzo Kila Kona Kinshasa

MASHABIKI wa soka jijini hapa wanazungumzia zaidi uwepo wa Bernard Morrison na Chris Mugalu kwenye kikosi cha Simba kitakachowavaa AS Vita Ijumaa saa 3 usiku.


Simba imetua Kinshasa na wachezaji 27 ili kujiweka tayari kwa lolote linaloweza kutokea hata kama baadhi yao watakumbana na mizengwe ya ugonjwa wowote.


Kwa mujibu wa mchambuzi na mtangazaji mahiri wa michezo kwenye redio maarufu ya Top Congo FM, Jenovic Mbowa wachezaji hao wawili ndio wanaosemwa sana na wanapewa nafasi kubwa ya kusumbua kwa vile wanaielewa vizuri DR Congo na aina ya soka na mambo ya ndani na nje ya uwanja.


Alisema Morrison kama akiongeza umakini kwenye kufunga ndiye anayeweza kuwa na madhara zaidi ndani katika mechi hiyo kwa vile wanamjua.


“Mugalu ni mchezaji mzuri na isitoshe ni Mkongo, anaelewa mambo mengi ya hapa kwa vile alicheza sana FC Lupopo ya Lubumbashi anawajua sana Vita, atasumbua,” alisema Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments