Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Mshirika wa Muimbaji R Kelly Ashikwa Akitaka Kumuhonga Shahidi Bilioni Moja ili Asitoe Ushahidi Dhidi ya R Kelly


 Richard Arline Jr. ambae ni mmoja wa Washirika wa R.Kelly amepatikana na hatia ya kujaribu kumhonga Mwanamke mmoja ili asitoe ushahidi dhidi ya R.Kelly Mahakamani.


Inaaminika Mwanamke huyo ni miongoni mwa Wanawake ambao R.Kelly alishiriki nao mapenzi kabla ya umri sahihi na ana siri nyingi za Mwimbaji huyo ambapo kwenye sauti za ushahidi zilizopatikana, Richard alisikika akimwambia Mwanamke huyo kwamba atampatia $500,000 (Tsh. Bilioni 1.1) ili akatae kwenda kutoa ushahidi Mahakamani dhidi ya R.Kelly.


Richard ni miongoni mwa Wanaume watatu ambao wameshitakiwa kwa kujaribu kuharibu ushahidi wa Mashahidi dhidi ya kesi ya R.Kelly ambapo June 2021 hukumu ya Richard itatolewa na kifungo cha kosa kama lake kinaweza kufikia hadi miaka 15 jela.

 DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL HAPA KUPATA HI
ZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE

R.Kelly (54) amekua akishikiliwa gerezani na kunyimwa dhamana wakati akisubiri kusikilizwa kwa kesi yake akidaiwa kuongoza kundi la Uhalifu kwa muda mrefu kusajili Wanawake na Wasichana na kufanya nao mapenzi.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments