Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Mtandao wa Spotify Kuzinduliwa Afrika Mashariki

MTANDAO  wa Spotify unatarajiwa kuzindua huduma zake katika masoko 85 mapya katika hatua ambayo itawafikia watu zaidi ya bilioni moja. Tangazo hilo lilitolewa kupitia hafla iliyoonyeshwa mubashara kupitia mtandao ikiwajumuisha na Justin Bieber, Prince Harry na Meghan Markle.

 

 

Spotify pia imetangaza huduma mpya ya usajili wa ubora wa juu wa sauti na soko jipya la matangazo ya podcast. Baadhi ya masoko mapya ya mtandao huo yako katika nchi zinazoendelea barani Asia, Afrika, Pacific na Caribbean.

 

 

“Masoko haya kwa pamoja yanawakilisha zaidi ya watu bilioni moja, nusu yao tayari wanatumia intaneti,” msemaji wa Spotify Alex Norstrom, alisema.

 

 

“Maeneo mengine tunayopeleka huduma zetu kama Bangladesh, Pakistan na Nigeria yana ukuaji wa haraka wa intaneti duniani,” aliongeza. Upanuzi wa awali wa mtandao huo nchini India, Urusi na Mashariki ya Kati tayari umewavutia mamilioni ya wafuatiliaji.

 

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments