Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Mtangazaji Aporwa Simu kwa Bunduki Hadharani
MTANGAZAJI wa televisheni wa kampuni ya DIRECTTV, Diego Ordinhola, nchini Ecuador, alijikuta akikingiwa bastola na mtu nje ya Uwanja wa Monumental huko Tarqui, Guayaquil, ambaye alimpora simu yake na kukimbia.

 

 

Ordinhola ameliweka wazi tukio hilo kwenye akaunti yake ya Twitter ya Februari 12, 2021, ambayo imeonwa na watu zaidi ya 350,000  na polisi wakiapa kumtia mbaroni mhusika au walioshirikiana naye.

 Katika picha iliyonaswa ya tukio hilo, mporaji anasikika wazi akisema “Simu, nipe simu yako” ambapo baada ya kuikamata akakimbia akiwa amewaa kinyago.


Ordinola na wapiga picha wenzake, walimfukuza mporaji huyo ambayo tayari alikuwa amevuka mtaa wenye patashika nyingi na alipanda bodaboda ambapo kamera zilimnasa akiwa anakimbia  na simu aliyoipora.


Mwaka jana ripota wa televisheni, Diego Demarco, alivamia na kuibiwa simu kabla ya kuanza kurusha matangazo mubashara jijini Buenos Aires, Argentina. Hata hivyo, watu waliokuwa jirani, wakiwemo watoto, walimfukuza mtu huyo wakamkamata na kumrudishia simu mtangazaji  huyo ambaye aliwamwagia shukurani nyingi.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments