Mtazamo wa wanaume 'bahili' na sikukuu ya Valentino

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA





Ulimwengu unapoadhimisha sikukuu ya wapendanao, ama Valentine, kuna kundi la wanaume wanaojiita 'bahili' walioibuka katika mitandao ya kijamii ambao kwao sikukuu hii ni mwiko.


Kote barani Afrika, makundi mbali mbali yameanza mchakato wa kuandaa 'makongamano' ya wanaume, ama makundi ya wanaume bahili, katika kipindi hiki cha sikukuu ya Valentine. Lakini lengo lao haswa ni nini?



Mwanahabari wetu Roncliffe Odit anaangazia chimbuko la makundi haya ya wanaume bahili, na kwa nini yana umaarufu mkubwa kote barani Afrika.



Kumekuwa na taarifa zilizotapakaa kuwa leo Jumapili Februari 14 ni siku ya pili ya Kongamano la Wanaume (Men's Conference).



Wajumbe kutoka mataifa mbali mbali waliwasili jana nchini Zambia, makao makuu ya Wanaume Bahali Afrika (Stingy Men Association of Africa). Uwepo wao hapa nchini Zambia ni kwa ajili ya kuhudhuria 'kongamano' kubwa zaidi barani Afrika, Kongamano la Wanaume, ambalo linaandaliwa kwa mara ya pili sasa.



Si sadfa kwamba 'kongamano' hili linakuja wakati ulimwengu ukiadhimisha Siku ya Wapendanao (Valentine's Day) inayoadhimishwa Februari 14 kila mwaka. Muungano wa Wanaume Mabahili umekuwa ukiandaa 'kongamano' hili kwa mwaka wa pili sasa ili kuwaepusha wanaume na sikukuu ya wapendao.



Ukweli ni kwamba hakuna 'kongamano' la ukweli linaloandaliwa huko Zambia. Lakini kutajwa kwa 'kongamano' hilo kumetumika ili kuwatenga wanaume mabahili na sikukuu ya Valentine.



Lakini kwa nini wanaume kuwa mabahili? Na mbona wanaume wanakataa kutumia hela zao wakati wa sikukuu ya wapendanao?



Mwangi Maina kutoka Kenya ni mwanahabari, na mshirika mkuu wa Kongamano la Wanaume.



Anasema wamelazimika kuja na 'kongamano' hilo ili kuzima mienendo ya kina dada kuwahadaa waume na kutumia hela zao wakati huu wa Valentine.



'Wanawake wengi ambao hawajaolewa hutumia sana sikukuu ya Valentines kufuja hela za wanaume. Ni lazima wakomeshwe,' anasema Maina.



Mwangi Maina pia ni muasisi wa mtandao wa Tutaoa Tukitaka (We Will Marry When We Want), ambao ni mtandao wa vijana wasio na haraka ya kufunga pingu za maisha. Na anasema sababu kubwa ya vijana wengi kutokuwa na haraka ya kuoa ni gharama kubwa inayohusishwa na mahusiano.



'Siku hizi mapenzi ni pesa, kama huna pesa hakuna msichana atakupenda. Kwa hiyo sisi tunatafuta pesa kwanza.'



Aidha maoni ya Mwangi Maina yanawakilisha asilimia kubwa ya wanaume kote barani Afrika ambao wameanza kujitenga na sikukuu ya wapendanao. Mitandaoni kumeibuka makundi mbali mbali ya wanaume bahili wanaojisifia kuwanyima hela wanawake.



Muungano wa Wanaume Bahili ulianzishwa na watumiaji wa mitandao ya kijamii nchini Zambia baada ya mwanamume mmoja kwa jina Leonard Mweembe kukamatwa kwa madai ya kumpiga mkewe aliyemuomba hela za kusuka nywele mwezi Novemba 2020.



Kufikia mwishoni mwa mwaka jana, matawi kadhaa ya muungano huo wa mtandaoni yalikuwa yameibuka katika mataifa mbali mbali barani Afrika.



Muungano wa Wanaume Bahili Tanzania, Muungano wa Wanaume bahili wa Kenya, Wanaume bahili wa Uganda, na kadhalika. Baadhi ya kauli mbiu zao ni pamoja na 'acha nione ninachoweza kufanya' 'natarajia hela fulani wiki ijayo' ,' nina issue ninasikilizia' ambayo ni misemo ya udhuru wa kuwanyima hela wapenzi wao au wake zao.



Mwanamuziki wa Nigeria Don Jazzy pamoja na muigizaji wa Kenya Desagu ni miongoni mwa watu mashuhuri ambao ni wanachama wa Muungano wa Wanaume Bahili Afrika.



Sikukuu ya Valentine huadhimishwa kila mwaka tarehe 14 Februari. Ni siku ambayo watu huonesha mapenzi kwa watu wao wa karibu kwa kuwatumia kadi, maua ama chokoleti zikiandamana na ujumbe wa mapenzi. Kitamaduni, wanaume ndio hutuma zawadi hizo kwa wanawake.



Wale wanaume mabahili wanaopinga maadhimisho haya wanahoji kwamba wanawake wamekuwa wakitumia siku hiyo kwa manufaa yao wenyewe. Baadhi ya wanaume hao wanadai kwamba mapenzi ni ya kila siku na hawafai kulazimishwa kutumia hela zao tarehe 14 Februari.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad