Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Muangola wa Yanga afunguka hatma yake

 


 KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Carlos Fernandes ‘Carlinhos’, amesema kuwa anamini kwamba atafanya vizuri ndani ya kikosi hicho kutokana na kutokuwa fiti kwa muda mrefu.

Ilikuwa inatajwa kuwa nyota huyo anahitaji kuondoka kikosini kutokana na kukosa nafasi ya kucheza ila ameweka wazi kwamba bado yupo.


Carlinhos aliyejiunga na Yanga msimu huu, kwenye usajili wa dirisha kubwa anapitia kipindi kigumu cha kujenga ushkaji na benchi kutokana na majeraha ambayo yamemfanya kuwa nje ya uwanja tangu Novemba mwaka jana.


Alisafiri na kikosi kuelekea Zanzibar kwenye Kombe la Mapinduzi ila arirejea Bongo kupewa matibabu na kwa sasa tayari ameshatengamaa afya yake.


Nyota huyo alianza vizuri msimu huu akihusika kwenye mabao manne ya Yanga, akifunga mawili na kuasisti mara mbili, lakini kwa sasa hasikiki kutokana na kutocheza kwa muda mrefu.


Raia huyo wa Angola amesema:"Nipo fiti kwa sasa kwa kuwa nilikuwa nasumbuliwa na majeraha hivyo kwa muda ambao nilikuwa sichezi kwa kuwa sikuwa fiti.


"Bado nipo ndani ya Yanga hivyo imani yangu ni kuona kwamba kila kitu kinakwenda sawa na mashabiki waendelee kutupa sapoti.


"Kuhusu kuanza ama kutokuanza kikosi cha kwanza hilo siwezi kuzungumzia kwa kuwa ni jukumu la benchi la ufundi, mimi ninachojua kwamba ni mchezaji wa Yanga na nitacheza nikipata nafasi," .


Yanga ipo nafasi ya kwanza kwenye msimamo ikiwa imekusanya jumla ya pointi 46 imefunga mabao 33 inafuatiwa na Simba iliyo nafasi ya pili na ina pointi 42.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments