Mume na mke wafariki siku moja Kilimanjaro katika mazingira tofauti

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA





Siha.Giza nene limetanda katika kijiji cha Wari, Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro, baada ya Mume na mke kufariki siku moja katika mazingira tofauti.

Tukio hilo ambalo bado limeacha maswali vichwani mwa wengi, lilitokea Februari 6, mwaka huu asubuhi, ambapo kifo cha mume kilisababishwa na ajali ya gari, huku mke wake akikutwa amefariki ndani ya nyumba.


 
Mwenyekiti wa kijiji hicho, Hamza Munisi,alikiri kutokea kwa vifo hivyo katika mazingira tofauti, ambapo aliyataja majina ya marehemu kuwa ni  Simon Emanueli, ambaye anakadiriwa kuwa na umri wa miaka 30 na Grece Mtolwa (27) na kwamba bado kumekuwa na giza juu ya chanzo cha kifo cha mke.

Akisimulia matukio hayo, Munisi alisema, asubuhi akiwa nyumbani, alipata taarifa za mtu kugongwa na gari maeneo ya dachikona karibu na shule ya msingi Gararagua.

“Nilipofika eneo la tukio, nilikuta tayari amefariki, nilipiga simu kituo cha polisi Sanya juu, ambapo walifika kuuchukua mwili na kwenda kuuhifadhi katika Hospitali ya Kibong’oto,” alisema Munisi.

Alieleza kuwa baada ya kuhifadhi mwili wa marehemu, alirudi nyumbani na wakati anakunywa chai alipata simu nyingine ikimjulisha kwamba kuna mama amekutwa ndani ya nyumba amefariki.

“Nilifika eneo la tukio na kukutana na mama mwenye nyumba, ambayo wawili hawa walikuwa wamepanga,ambaye alinieleza namna walivyobaini kifo cha mama huyo, na mpaka sasa bado chanzo hakijajulikana,” alieleza mwenyekiti huyo.

Kwa mujibu wa mama mwenye nyumba huyo, siku ya tukio, mtoto wa marehemu, ambaye ni mdogo, alitoka ndani akiwa amechafuka, akamuagiza mtoto mwingine kwenda kumuamsha mama yake ili aweze kumsafisha.

“Baada ya mtoto yule kwenda ndani, alirudi akasema anamwamsha mama yule lakini hakuamka, ikanilazimu niingie ndani mwenyewe kumuamsha ili amsafishe mtoto, lakini nilikuta amefariki,na hivyo nikatoa taarifa kwa mwenyekiti wa kijiji”alieleza mama huyo.

Ebenezery Mmari, ambaye ni baba mwenye nyumba, alisema taarifa za vifo hivyo vimewashtua na kwamba chanzo cha kifo cha mke bado hakijafahamika na kinachosubiriwa ni uchunguzi wa kitaalamu, ili kubaini chanzo chake.

 DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE



Kaimu kamanda wa polisi Mkoa wa Kilimanjaro Ronald Makona akizungumzia tukio hilo, alithibitisha kifo cha kijana mmoja katika Wilaya ya Hai, na kueleza kuwa tukio la Siha bado analifuatilia.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad