Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Mume wa Queen Darleen Afunguka Kumpendelea Mke Mdogo


MUME wa mwanamziki Queen Darleen, aitwaye Isihaka, leo Februari 9, 2021,  ametolea ufafanuzi suala la yeye kumpendelea mke mdogo (Darleen)  na kutomjali mke wake mkubwa anayefahamika kama Sabra.


Kupitia kipindi cha Mashamsham cha kituo cha radio ya Wasafi amesema siyo kwamba kweli kwamba anampendelea mke wake mdogo kama inavyosemekana mtandaoni ila kwa kuwa Queen ni msanii; akipost kitu kinaenda sana kuliko mke mkubwa na pia mke mkubwa ana vitu vingi kuliko mke mdogo kwa sababu ana magari lakini Queen hajamnunulia na mke mkubwa ana nyumba yake lakini mke mdogo amepanga.  Kwa hiyo siyo kwamba anampendelea mke mdogo.

“Sabra ndiyo ana siku nyingi za kuwa na mimi, ana siku nne, halafu Queen Darleen ana siku tatu za kuwa na mimi,” amesema Isihaka


 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments