Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Msukuma, ameiomba serikali kuanzisha dirisha maalum la kutoa mkopo kwa wahitimu wa elimu ya juu, ili kuwasaidia kupata fedha za kujiendeleza.
Musukuma ameyasema hayo bungeni leo Februari 8, 2021, ambapo pamoja na hilo amemuomba Rais Magufuli akutane na wafanyabiashara ili wajadili namna ya kunusuru biashara zinazofungwa kutokana na watu kushinda kuziendesha.
''Mimi naona cheti cha degree kitumike kama dhamana, serikali inatakiwa ianzishe dirisha la mikopo kwa wahitimu ili ifanye kama inavyofanya bodi ya mikopo ya elimu ya juu ambayo yenyewe inaamini ubongo tu inampa hela mwanafunzi kwanini sasa akihitimu degree yake isiaminiwe na akapewa mkopo kupitia hiyo'' - amesema Musukuma.
Aidha Musukuma amesema, ''kama ambavyo Rais Magufuli alitusikiliza watu wa madini, naomba pia akutane na wafanyabiashara wa kawaida ili ajue wanapitia nini na kwa pamoja wajadili namna ya kuwasaidia''.