Muziki wa Bongo Umekuwa Mgumu Sana.. Bila skendo Hutoboi


Muziki wa Bongo umekuwa mgumu sana.. Bila skendo kufanikiwa inakuwa ngumu sana.. Tena sana..

Juzi Nandy katoa nyimbo na Mopao.. Hit Song ya maana lakini nani anayejali?

Baada ya nyimbo hiyo, Harmonize na Kajala wakaweka mahaba yao hadharani... Insta yote ikahamia huku.. Online TV zote zikahamia huko..

Kama hiyo haitoshi, zimetoka video za Rayvanny na Paula.. Mji wote leo unawajadili wawili hawa.. Nyakati zimekwenda wapi?

Nani anajali tena kuhusu ngoma ya Nandy na Koffi? Hakuna.. Skendo zimeipeleka nyimbo kubwa kaburini.. Inakufa kifo cha kawaida..

Kwa kweli Bongo Fleva imekuwa ngumu.. Kwa sasa ili kutrend lazima ujiunge na makundi haya mawili.. Kama upo nje ya mfumo inabidi uwe mpambanaji kweli..

Rostam wametoa ngoma yao juzi.. Nyimbo kali wamemshirikisha Ben Pol.. Nani anajali kuhusu ngoma hii?

Kila mtu sasa anamjadili Kajala na mwanaye Paula... Inaumiza sana..

Tunawapoteza wasanii wengi wazuri kutokana na mahitaji ya muziki wa sasa..

Muziki wa sasa hauhitaji ujue kuimba sana.. Ni zaidi ya kuimba.. Ujue kucheza na hizi skendo.. Bila hivyo hutoboi..

By Gift Macha

 DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE