Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Mwanamuziki Bow Wow Kuingilia Mieleka
Mwanamuziki wa mtindo wa rap kutoka nchini Marekani Bow Wow wa miaka 33 ametangaza kwamba atajiunga na kipindi cha mieleka WWE ambapo naye pia atakuwa akipigana.

Alitangaza haya kupitia Twitter jana Jumatatu ambapo alisema alijua kwamba wengi watashangazwa na uamuzi wake lakini ameshachagua.

Kulingana naye amekuwa na hamu ya kupigana mieleka tangu utotoni. Mwanamuziki huyo amesema kwamba yuko karibu kuzindua albamu yake ya mwisho na baada ya hapo ataangazia tu maswala ya televisheni, filamu na WWE.


Ili kuonyesha kwamba yuko makini kuingia WWE, Bow Wow aliandika kwamba ameshachagua kundi la mpiga mieleka Rey Mysterio na anatumai kushirikiana naye kwenye mashindano ya mieleka siku za usoni.

Albamu hiyo yake ya mwisho, Bow Wow ameipa jina la “Before 30” huku akisema kwamba alichagua jina hilo kwa mkusanyiko wa vibao vyake kumi kwani yote ambayo ametimiza maishani kufikia sasa aliyaona kabla ya kutimiza umri wa miaka 30.

Wakati wa mahojiano mwezi Januari mwaka huu kwenye kituo cha redio cha Marekani kwa jina Hot 97, Bow Wow alisema kwamba atamhusisha mwanamuziki Snoop Dog kwenye albamu hiyo kama msimulizi.

Awali Bow Wow alikuwa akijiita Lil Bow Wow katika ulingo wa muziki na jina lake halisi ni Shad Gregory Moss. Alizaliwa mwezi Machi mwaka 1987 na akaanza kazi ya muziki mwaka 1993 huku akiingilia uigizaji mwaka 2001.


Amewahi kuigiza kwenye filamu kadhaa na kwenye vipindi vya runinga wakati mwingine kama mhusika mkuu na kwingine kama mhusika mdogo.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments