Patashika ya kombe la dunia la FIFA Qatar


Kombe la  Dunia kwa vilabu bingwa wa mabara  yanaanza leo tarehe 4/02/2021 hadi 11/02/2021 nchini Qatar, katika viwanja vitatu tofauti Ahmad bin Ali, Education City na Khalifa International.


Michuano hii, hukutanisha mabingwa wa mashirikisho ya mabara yote 7, kama UEFA, CAF CONMEBOL ,AFC, CONCACAF na OFC ambapo Africa tunawakilishwa na Al  Ahly ya Misri.Fungua dimba itahusisha  mechi mbili,  Tigres UANL  dhidi ya Ulsan Hyundai na ile ya pili itakuwa  AL Duhail na Al Ahly ambao  ndio wawakilishi kutoka bara la Africa wakiwa na uzoefu  mkubwa wa kushiriki mashindano hayo.Katika timu ya Al Duhail yupo mchezaji  Michael Olunga raia wa Kenya anayecheza soka la kulipwa huko,ambapo mshindi wa mechi hii atakutana na mabingwa wa Ulaya kutoka shirikisho la UEFA ambao ni  Bayern Munich.Bayern Munich wanatarajiwa kuwa mabingwa kama ilivyo desturi ya washindi kutoka katika shirikisho la UEFA, ambaye hadi sasa bingwa mtetezi ni Liverpool, huku Real Madrid akiongoza kwa kutwaa ubingwa mara 4, Barcelona 3.Munich wanaonekana kuyapa mashindano haya kipaumbele cha hali ya juu kwa kuorodhesha  wachezaji wake bora  kama Thomas Muller, Manuel Neuer na Robert Lewandowski miongoni wa majina 23 yanayotakiwa.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE