Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Kimenuka...Unaambiwa PCK Atishia Kumburuza Wema Kortini

UNAMKUBUKAyule future husband (mume mtarajiwa) wa staa wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu ‘Tanzanian Sweetheart’ aitwaye Patrick Christopher ‘PCK’, ameibuka upya akitishia kumburuza kortini mwanadada huyo.

 

PCK ambaye ni promota na msanii wa muziki wa Kizazi Kipya kutoka nchini Burundi aliwahi kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na Wema kipindi kile ilipovuja video yao ya mambo ya chumbani kabla ya kumwagana yapata miaka miwili iliyopita.Akizungumza na Gazeti la IJUMAA kwa njia ya WhatsApp akiwa Kampala nchini Uganda, PCK ameibuka na madai mapya kwamba, anamdai Wema gari alilompa enzi za mahaba motomoto aina ya Jeep Infinity, toleo la mwaka 2010 hivyo ananuia kumburuza kortini.

 

PCK anadai kuwa, wakati akiwa na Wema, mahaba yao yalikuwa ni ya moto mno kwani walipendana kwa dhati na ilikuwa kimyakimya hivyo waliahidiana vitu vingi ikiwemo ishu ya kumuoa hivyo kumpa vitu kama gari halikuwa tatizo.“Nilimfanyia vitu vingi tu, nilimpeleka hadi China kipindi kile aanafungua duka la nguo za watoto.

 

“Pia tulinunua kiwanja kule Kigamboni (Dar) ambacho sijui mpaka sasa hivi kama alikiendeleza au ni nini kinaendelea maana nilimpa kama mwanamke wa maisha yangu.“Lakini sasa hivi ninajutia kuwa na Wema kwa sababu ya mambo yaliyotokea baadaye.“

 

Kuhusu gari nadhani watu wengi wanakumbuka lile gari ambalo Aunt Ezekiel alisema alimzawadia Wema, lakini ukweli lile gari nilinunua mimi na lina jina langu.“Nimekuwa nikimwambia anirudishie tu gari langu, lakini naona hanielewi hivyo nimeamua kufuata taratibu za kisheria.

 DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


“Siyo Wema tu, kuna kigogo mwingine mkubwa tu Tanzania ambaye naye ninamdai gari aina ya Land Cruiser V8, toleo la mwaka 2017,” anasema.Kwa upande wake, Wema amekuwa hataki kumzungumzia jamaa huyo kwa sababu anahisi ni mtu aliyetumwa kwake kwa ajili ya kumharibia maisha yake.

GPL

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments