2/14/2021

Pogba Ampasua Kichwa Solskjaer
KOCHA wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer, amefunguka kuwa staa wake Paul Pogba ataendelea kuwa nje, huku beki Eric Bailly huenda akarejea uwanjani.

 

Leo Jumapili, Man United itakuwa ugenini ikicheza dhidi ya West Brom katika mchezo wa Premier League.

 

Pogba aliumia hivi karibuni walipocheza dhidi ya Everton kwenye sare ya 3-3, alikosekana kwenye mchezo wa FA dhidi ya West Ham.Solskjaer alisema: “Paul ataendelea kuwa nje na natamani apone haraka na kurejea uwanjani, lakini Bailly amefanya mazoezi, hivyo kwa upande wake linaweza kutokea lolote kulekea mchezo wa kesho (leo).“Ni wachezaji muhimu lakini hali zao ndiyo ziko hivyo.

 

Tunaenda kucheza, tunahitaji kupata matokeo mazuri ili kuwa kwenye nafasi nzuri kwa sababu kama ukipoteza hata pointi moja itakuwa ni tatizo kwa upande wetu.“

 

Kitendo cha kupoteza pointi mbili dhidi ya Everton sikukipenda na sitaki kuona kinajirudia tena ndiyo maana nimewandaa vijana wangu kwa kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa.”

 

Ukiachana na mchezo huo kati ya Man United na West Brom, mechi zingine leo Jumapili ni Arsenal v Leeds, Southampton v Wolves na Everton v Fulham

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger