Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Poshy Aanika Ukweli Kumfumania Mumewe

MWANAMAMA mjasiriamali mwenye umbo matata ambaye ni maarufu kwenye mitandao ya kijamii Bongo, Jacqueline Obeid ‘Poshy Queen’, ameanika ukweli juu ya madai mazito kwamba wiki kadhaa zilizopita alimfumania mumewe ambaye ni raia wa Nigeria anayejulikana kwa jina moja la John.

 

Katikati ya mwezi Januari, mwaka huu; miezi mitatu baada ya Poshy Queen kujifungua, zilienea tetesi za mitandaoni kwamba alimfumania mumewe huyo na kilichofuata, wakaachana.

 

Ilisemekana kwamba, mwanamama Poshy Queen alimfumania jamaa huyo na staa mmoja wa Bongo Movies ambaye hakutajwa.Itakumbukwa kwamba, baada ya Poshy Queen kuchumbiwa na mwanaume huyo ambaye ana pesa zake aliahidi kutulia na kujenga familia yake ikiwemo kumzalia jamaa huyo watoto.

 

Akifunguka juu ya ishu hiyo, Poshy Queen anasema kuwa, hajawahi kuachana na mume wake huyo kama ambavyo watu wengi walieneza kwenye mitandaoni ya kijamii.Mwanamama huyo anaendelea kusema kuwa, alishangaa kuona jinsi watu wanavyosema kuwa ameamua kuachana na mume wake kwa sababu alimfumania, jambo ambalo siyo kweli.

 

“Sijawahi kumfumania mume wangu na mwanamke mwingine na wala sijaachana naye.“Bado tupo pamoja, sasa nashangaa jinsi watu wanavyosema huko mitandaoni kuwa nimeachana naye, nawashauri tu wafanye mambo yao, waache kuingilia familia za watu,” anasema Poshy Queen akiweka sawa juu ya skendo hiyo.

 

Julai 18, 2020, Poshy Queen alivishwa pete ya uchumba na John ambapo Novemba, mwaka jana, walibahatika kujaaliwa mtoto wao kwa kwanza.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments