Profesa Mkenda: Tutawashughulikia Watakaokwamisha Uzalishaji Sukari

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


Serikali imebaini mbinu chafu za watu kukwamisha uanzishaji wa viwanda vipya vya sukari ili kupunguza uhaba wa sukari unaojitokeza mara kwa mara nchini.

Akizungumza na Wakulima wa miwa katika bonde la Mbigiri Wilayani Kilosa,mkoani Morogoro Waziri wa Kilimo Profesa Adolf Mkenda amesema serikali imegundua na imejipanga kukabiliana na njama hizo ili kuhakikisha viwanda vingi vinaanzishwa ili kuongeza ushindani katika soko la miwa kwa wakulima.

Profesa Mkenda amesema licha ya uzalishaji wa miwa kuwa mkubwa lakini Tanzania bado inaupungufu wa sukari na tatizo likitajwa ni uwezo mdogo wa viwanda vilivyopo  kuchakata miwa hiyo kutoka kwa wakulima.

"Niwaombe wale wote wanaotaka kuanzisha viwanda vya sukari waje kufanya hivyo na serikali tutawalinda,na yeyote atakayekwamisha tutashughulika nae."Alisisitiza Prof.Mkenda.

Waziri Prof.Mkenda amemaliza ziara yake ya siku tatu ya kutembelea wakulima wa miwa na uongozi wa viwanda vya sukari mkoani Morogoro kuangalia namna bora ya kuendeleaza zao la miwa ili kupunguza nakisi ya sukari ya tani 40,000 ambayo Tanzania uagiza kutoka nje.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad