Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Rais Joe Biden wa Marekani Aomba Bunge Kubadili Sheria ya Ununuzi wa Silaha Marekani


Rais Joe Biden wa Marekani jana ameliomba Bunge kufanyia mageuzi sheria ya ununuzi wa silaha Nchini humo, amesema hayo kwenye taarifa yake wakati wa kumbukumbu ya miaka mitatu tangu tukio la ufyatuaji risasi Shuleni Florida na lililosababisha vifo vya Watu 17.


Biden amewataka Wabunge kupitisha Sheria itakayowalazimu Wanunuzi wa silaha kuchunguzwa kwanza historia zao pamoja na kuzuia uuzwaji wa silaha za mashambulizi na zenye uwezo wa kuchukua idadi kubwa ya risasi.


Mshambuliaji kwenye tukio hilo la Parkland Nikolas Cruz, alikuwa na bunduki aina ya AR-15 wakati aliposhambulia Watu kwenye Shule ya Marjory Stoneman Douglas aliyokuwa akisoma, ingawa alikuwa akijulikana kuwa na tatizo la akili lakini bado alifanikiwa kununua silaha kihalali

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments