Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Rais Magufuli 'Maalim Seif Alikubali Maridhiano, na Alikuja Chato na Rais Mwinyi, Mazungumzo yake yalikuwa ya Raha Sana Mungu Ampokee'

 


 “Natoa pole kwa Watanzania wote kwa vifo vyote viwili, cha Maalim Seif pamoja na cha Balozi Kijazi, Jana nilimtuma Makamu wa Rais na Dkt. Bashiru waniwakilishe kwenye mazishi ya Maalim Seif”-JPM kwenye shughuli za kumuaga Kijazi

“Baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 Maalim Seif aliniandikia barua mara tatu tofauti, baadaye nikaona nionane nae alipokuja akaniambia sijashiriki kwenye Uchaguzi ila sitohamasisha vurugu, Zanzibar itakuwa kwenye Amani,na nilithibitisha hilo kwa vitendo” Rais MAGUFULI


“Hata baada ya Uchaguzi wa Mwaka 2020, Maalim Seif alikubali maridhiano, na alikuja Chato na Rais Mwinyi, mazungumzo yake yalikuwa ya raha sana, Maalim alikuwa mcheshi, alikuwa akihubiri umoja wa Wazanzibar na Watanzania, Mungu ampokee mahali pema peponi” Rais MAGUFULI

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments