Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Rais Magufuli 'Sio Kila Dawa Inayotoka Nje ni Kwa Ajili Yetu..Tusitumike'

Rais Magufuli 'Sio Kila Dawa Inayotoka Nje ni Kwa Ajili Yetu..Tusitumike'Rais Dkt. John Magufuli amewataka watanzania kutumia dawa za asili katika mapambano dhidi ya Covid-19

Akizungumza Jijini Dodoma leo, amesisita juu ya matumizi ya miti shamba pia kujifukiza katika mapambano dhidi ya Covid-19.

Aidha amesema kuwa si kila dawa zinazotoka nje ya nchi ni nzuri kwa watanzania.

''Kuna dawa inaitwa Covidol, Bugiji zinafanya kazi kwasababu zimekua proved na mkemia mkuu, kamwe msifikirie kila dawa inayotoka nje ni kwa ajili yenu, ingekua hivyo Malaria ingeisha. Tujitaambue tusitumike. Madawa haya yalipigwa vita na wakoloni kwasasab ya uchumu, ukiw ana mti wako hata kama unaponesha malaria utaambiwa ni wa kishamba''. Alisema Magufuli

''Mungu ametuma hii mimea na ikabarikiwa, tuitumie, lakini tuitumie kwa kufuata masharti na utaalamu mzuri, kwa hiyo Taasisi yetu ya Wizara ya Afya inayosimamia dawa za asili, huu ni wakati wa kuyatumia kikamilifu. Na Wizara ya Afya isiwakatishe tamaa watu hawa, na madaktari wanatumia hizo hizo dawa, wao wanaenda wanakunywa, wanajifukiza wakija huku wanawatwanga masindano'' - Rais Magufuli


 DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA HUNA  BUNDLE

 

Ameongeza pia kuwa Watanzania kwa wakati wote wamemtanguliza Mungu na kuendelea kujilinda hivyo wanapaswa kuendelea kuchukua tafadhali.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments