Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Rapper Offset Amnunulia Zawadi ya Mkoba Card B Wenye Thamani ya Milion 47 Siku ya Valentines Day

 


Ni zawadi gani mpendwa wako amekupatia jana kwenye siku adhimu ya wapendanao? Au jana mambo hayajawa mambo tuisikilizie Valentine ya 2022?


Wakati ukichukulia poa siku hii, huko Marekani rapa Offset hakuwa na dogo kwa Baby Mama wake Cardi B hapo jana, kwani amempatia CardiB zawadi ya mkoba ulio ndani ya kifungashio maalum ukijulikana kama (Cage Bag) wenye thamani ya $ 20,500 ambazo sawa na Tsh Milioni 47,539,500.


CardiB ametoa shukrani za dhati kwa mumewe kwa zawadi hiyo ya kitofauti ambayo hakuitegemea, sambamba na kuonyesha mkoba huo pamoja na bei kupitia risiti ya manunuzi.


“Wow Asante mpenzi (Offset). Mara nyingi unaniletea vitu vya kitofauti nakupenda na nakuheshimu sana”. Aliandika CardiB kupitia ukurasa wake wa Ig.


Hii sio mara ya kwanza kwa Offset kumnunulia mkewe zawadi za mtonyo mrefu. Kwani miezi minne iliyopita Baby Dad wake huyo alimzawadia gari la zaidi ya Sh. Bilioni 1.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments