Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Simba na Biashara United Kuvaana leo, Hawa Hapa Nyota wa Simba Wataoukosa Mchezo huo
UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa upo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Biashara United utakaochezwa leo Februari 18.
Mchezo wa leo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili kutokana na mipango ya makocha kuhitaji ushindi.

Francis Baraza, Kocha Mkuu wa Biashara United anahitaji kulipa kisasi cha kufungwa mabao 4-0 kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Kwenye mchezo huo nyota wa Simba, Luis Miquissone aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kupiga hat trick ya asisti ambazo ni tatu.

Didier Gomes, Kocha Mkuu wa Simba amesema anahitaji pointi tatu ili kupunguza gape la pointi saba anazodaiwa na Yanga inayoongoza Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 46 baada ya kucheza mechi 20.

Simba imecheza mechi 17 ina pointi 39 ikiwa nafasi ya pili msimu wa 2020/21.

Simba inatarajiwa kukosa huduma ya nahodha, John Bocco ambaye ni majeraha pamoja na kiungo Jonas Mkude.

Haji Manara, Ofisa Habari wa Simba amesema kuwa wamejipanga na wapo tayari kupata matokeo mazuri ndani ya Uwanja wa Karume, Mara.

"Kila kitu kipo sawa na tunatambua kwamba utakuwa mchezo mgumu ila tunahitaji pointi tatu ndani ya uwanja,".

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments