2/20/2021

Simba "Tunakusudia Kufikia Nusu Fainali ya Mashindano"

 Kuelekea mchezo wa Klabu bingwa barani #Afrika kati ya Simba na Al Ahly ya Misri, Msemaji wa Klabu hiyo, Haji Manara amesema Simba ina historia nzuri ya kushinda inapokutana na Al ahly katika Ardhi ya Tanzania


Mchezo huo ambao utapigwa siku ya Jumanne tarehe 23 Februari 2021 umebeba kauli mbiu ya 'TOTAL WAR , POINT OF NO RETURN'. Manara asema wanao uwezo wa kuwafunga kwasababu Simba hupenda mechi kubwa kama hizo


Amesema kuwa, 'target' yao ya chini ni kufika nusu fainali ya michuano hiyo. "Ni vita ya nje na ndani ya uwanja lazima tupate point 3. Wachezaji wanaenda kucheza kuwakilisha Simba, #Tanzania na ukanda wote wa Afrika Mashariki".


 

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger